
NO.
0001
MRISHO
S. MBWEMBWE (ABU WARDA)
Blog:
academiccharity.blogspot.com
Likomale.
blogspot.com
Phone:
0657-942497
E-mail:
mrishombwembwe@gmail.com
Utangulizi:
Leo katika uga huu wa FIKRA MPYA napenda
kuwaletea makala ambayo itasaidia kuamsha hari, hamasa na fikra chanya kwa kila
atakayebahatika kuisoma habari hii. Ni dhana mpya ambayo itaogeza udadisi na
mabadiliko chanya kwenye jamii yetu ambayo tunahitaji ibadilike na kusonga
mbele siku hadi siku.
DHANA YA MTAJI KATIKA UJASIRIAMALI
AU BIASHARA.
Ndugu zangu, natumaini sote tunajua kuwa
ukimuuliza mtu kuhusu suala la mtaji au “kwanini unashindwa kufanya biashara au
shughuli fulani ya Ujasiriamali?”; ni dhahiri kuwa 90% au zaidi ya watu
watakwambia kuwa “Sina Mtaji” ndio maana nashindwa kuanzisha biashara au
Ujasiriamali. Na asilimia hiyo ya wanaojibu hivyo huwa wanamaanisha kuwa “HAWANA
PESA au HELA”!!! Hii inamaanisha kuwa dhana ya mtaji inaeleweka
kwa kiasi kikubwa au watu wengi kuwa ni PESA. Mbaya zaidi, dhana hii imedumaza
fikra zetu kwa kiasi kikubwa na kutufanya wengi tubweteke na tushindwe kuchukua
maamuzi sahihi.
FIKRA MPYA…………………………….
Ukweli ni kwamba; ingawa pesa ni muhimu katika
biashara au ujasiriamali; si kweli kwamba pesa ndio mtaji mkuu!!!!! Pesa
inachukua nafasi ya chini katika mtaji kwa kuwa kuna rasilimali (Mitaji) ambazo
kama mtu hatokuwa nazo, basi hata awe na pesa kiasi gani- itakuwa ni sawa na
kutwanga maji kwenye kinu! Kwa ufupi, Mitaji na Rasilimali za msingi kabla ya
pesa ni:
1.
Akili/Fikra
(Mindset)
2.
Nia/Kuchukua
maamuzi (Will)
3.
Rasilimali
watu/Nguvu (Human Resources)
4.
Matumizi
chanya ya Urafiki au Familia (Roundtable Empowerment System-RES)
5.
Ufahamu
sahihi (Knowledge)
6.
Uthubutu na
kuchukua hatua (Positive Decision)
7.
Pesa/Hela
(Money)
·
Kama
tuonavyo hapo juu. Pesa imechukua nafasi ya SABA na si ya KWANZA! Hii ndio
sababu kuwa Pesa ni muhimu katika biashara au ujasiriamali lakini sio Msingi.
Kuna mambo ambayo tunayakosa ndio maana tumebaki kwenye lindi la kusingizia
kuwa hatuna mtaji wakati tuna fursa kubwa ya mtaji ambao yunashinda kuutumia.
Nia ya FIKRA MPYA si kulaumiana au kushutumiana bali ni kuamshana na kuamsha
hisia chanya zenye kuweza kutubeba kutoka hapa tulipo na kutupeleka hatua
kadhaa mbele. Katika toleo lijalo (Namba 0002) nitawafafanulia jinsi gani fursa
namba 1 hadi 6 hapo juu zinavyoweza kufanya kazi kwa muujiza mkubwa hatua kwa
hatua…………………………………………………………………….
Hadi
toleo lijalo (Mwenyezi-Mungu Akipenda); Kumbuka FIKRA MPYA- “Fikiri na Tazama
kwa Jicho la Tatu.”………………………………………………
NO. 0002
MRISHO
S. MBWEMBWE (ABU WARDA)
Blog:
academiccharity.blogspot.com
Likomale.
blogspot.com
Phone:
0657-942497
FIKRA MPYA KUHUSU MTAJI NA VYANZO
VYA UJASIRIAMALI NA BIASHARA
Habari za weekend ndugu zangu; leo tena
tunakutana katika uga huu wa FIKRA MPYA ili kuendelea kushirikishana katika
kupeana maarifa kama sehemu ya maendeleo yetu katika jamii. Kama tunakumbuka
vyema, wiki iliyopita tulianza kuzungumzia dhana ya mtaji ambayo wengi tunadhani
kuwa PESA ndio mtaji mkuu; lakini nilieleza kuwa kuna mambo mengine tangulizi
ambayo ni mitaji mikubwa kuliko pesa- naomba twende pamoja ili niyafafanue:
1.
AKILI/FIKRA
(MINDSET)
Fikra ndio kitivo kikuu cha
utendaji wa mtu. Ujasiriamali huanza na FIKRA na AKILI ya mtu; kwa mfano; mtu
anapowaza kuwa ana uwezo wa kufanya jambo fulani la kijasiriamali, basi huo
ndio msingi wa Mtaji wake. Hii ni tofauti na yule ambaye kila mnapozungumza
kuhusu biashara anakwambia kuwa yeye hawezi na anaamini kuwa kuna watu maalum
walioumbwa kwa ajili hiyo.
2.
NIA/KUCHUKUA
MAAMUZI/DHAMIRA (WILL)
Dhamira ni msingi wa pili wa
ujasiriamali. Dhamira ni mfano wa mtu kuamua kuitumia bunduki aliyonayo ili
aweze kulenga na kupiga mnyama. Hivyo, Dhamira ni mtaji muhimu sana katika
shughuli ya kimaendeleo.
3.
RASILIMALI
WATU/NGUVU (HUMAN RESOURCES)
Mtu au watu ni mtaji muhimu wa
kufanikisha shughuli ya ujasiriamali. Mtu mmoja anaweza kuongeza nguvu kwa
kumshirikisha ndugu au rafiki mwenye mawazo yanayofanana na yake ili kuanzisha
na kuendesha ujasiriamali.
4.
MATUMIZI
CHANYA YA URAFIKI AU FAMILIA (ROUNDTABLE EMPOWERMENT SYSTEM- RES)
Dhana hii ni mpya na muhimu
sana katika jamii zetu. Dhana hii inaelezea jinsi ya kubadili mazoea yasiyo na
“faida” na kuwa mtaji wenye kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yetu!
Kwa mfano; ni dhahiri kuwa, marafiki na ndugu huwa tunachangiana kiasi kikubwa
cha pesa kwenye shughuli mbalimbali kama vile; Harusi, Send-off, Birthday,
Graduation, Kitchen Party, Ngoma, “Beseni” n.k.! Kwa ufupi ndugu zangu;
tunaweza kubadilisha au kuboresha mazoea haya kuwa mtaji wa Ujasiriamali mkubwa
sana! Vilevile, tunafahamu kuwa watu huchangia kiasi kikubwa cha fedha katika
shughuli hizi- hadi kufikia kiasi cha elfu 60 (single) au laki moja (100,000-
double)!! Tuchukulie mfano kuwa katika marafiki na ndugu tunaochangiana
tunafikia 50 tu; tuamue kuwa tunataka kuanzisha mfumo wa kuwezeshana kimzunguko
(Roundtable Empowerment System-RES) ili kila mmoja
kati yetu aweze kuanzisha biashara. Pia tuchukulie mfano mdogo kuwa kila baada
ya mwenzi mmoja au miwili tunamchangia mwenzetu mmoja shilingi elfu ishirini
(20,000/=) tu kutoka kila mmoja wetu; kwa ufupi anayechangiwa atapata shilingi
milioni moja (1000, 000/=)! Kwa kanuni za ujasiriamali; kiasi hicho cha pesa ni
kikubwa saaana kuwa mtaji- haswa ukiangalia historia ya wajasiriamali wengi
duniani ambao walianza na mtaji na biashara ndogo saana! Njia hii ya
kuchangiana itazalisha jamii yenye uwezo mkubwa sana wa kusaidiana kwa kuwa na
uwezo zaidi
kiuchumi.
5.
UFAHAMU
SAHIHI (KNOWLEDGE)
Ufahamu sahihi kuhusu biashara
ya kufanya ni mtaji muhimu sana kuliko pesa. Ni vyema tukaanza na kuongea au
kuomba ushauri kwawale ambao wameshaanza au kupitia shughuli ambayo unataka
kuifanya- hii itasaidia kukupa ufahamu sahihi kabla ya kuanza.
6.
UTHUBUTU
NA KUCHUKUA HATUA (POSITIVE DECISION)
Ndugu yangu; baada ya kuwa na
yote hapo juu, kinachofuata ni kuchukua hatua ya kuanza shughuli yako ya
ujasiriamali. Tukumbuke kuwa; kwenye jamii kuna watu wengi wenye ndoto lakini
wanachoshindwa ni kuchukua hatua ya kuanza kutembea kwenye ndoto yake
kimatendo. Kutokana na hili; wengi husema-“ Utajiri uko kaburini kwa kuwa wengi
wanakufa na ndoto zao”.
7.
PESA/HELA
(MONEY)
Naomba tukubaliane kuwa; pesa
inashika nafasi ya saba kwa kuwa hata kama mtu ana pesa, pasipo kuwa na mambo
yaliyotangulia ni kazi bure. Hii ndio sababu ya watu wengi waliotegemea na
kutumia pesa zao kama mtaji na mwisho wakaua biashara zao!
Hadi
toleo lijalo (Mwenyezi-Mungu Akipenda); Kumbuka FIKRA MPYA- “Fikiri na Tazama
kwa Jicho la Tatu.”………………………………………………
No comments:
Post a Comment